Ripoti ya ABNA- Idadi hiyo ya vifo imeongezeka kwa zaidi ya watu 200 baada ya takwimu zilizotolewa jana jioni na wizara ya afya ya Misri zinazoonyesha kuwa karibu watu 235 wameuawa na wengine 2,000 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea nchini humo. Wizara hiyo pia imesema, askari 43 wameuawa katika mapigano hayo.
16 Agosti 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 452538
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema, karibu watu 421 wameuawa na wengine 3572 kujeruhiwa katika mapigano kati ya wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi na vikosi vya usalama, baada ya vikosi hivyo kuwatawanya waandamanaji hao katika maeneo mawili ya maandamano nchini Misri.